Posts

THERE IS NO FUTURE IN THE PAST

Image
THERE IS NO FUTURE IN THE PAST. Ukitaka kufanikiwa usiangalie nyuma yako kunanini na ulishindwa mara ngapi. Siku zote kukaa Chini nakuanza kujuta kwa makosa uliofanya uko nyuma nikupoteza muda, huo muda Utumie kwa kupanga ya kesho. Bahati nzuri Mungu alitujalia kusahau, ivyo siku zote sahau ya nyuma na waza yale ya mbele yako. Maisha bora ya mbele hayawezi kuja kama akili yako imebeba kushindwa kwa nyuma. Binadamu yeyote anayeweza kupoteza muda wake wa leo kwa kulaumu mabaya ya jana, kesho atapoteza muda akilaumu mabaya ya leo. Tambua ya kuwa, "hakuna awezaye kurudi nyuma na kuanza upya, bali waweza kuanza leo na kutengeneza maisha yako ya kesho" Kadri unavyofikiria ya nyuma ndivyo unavyochelewa kufika mbele zaidi. Penda zaidi ndoto yako ya kesho kuliko historia yako ya jana,maana hatima yako siku zote iko mbele na sio nyuma. Siku zote utashindwa kwa kuendekeza mambo yaliopitwa na wakati maana utakuwa unatumia ujuzi uliopitwa na wakati. "Habari njema ya siku ni ...

FAIDA ZA MMEA WA GINSENG

Image
FAIDA ZA MMEA WA GINSENG. Ginseng ,au maarufu kama “king of herb” (mfalme wa mimea). Mmea huu umekuwa moja ya maajabu ya dunia kutokana na uhodari wake katika matibabu.  Mmea huu unapatikana hasa kaskazini  mwa America na Mashariki mwa Asia(hasa kaskazini mwa china,Japani na Korea) hasa maeneo yenye baridi. Kuna aina kuu mbili za mmea huu : American Ginseng(Panax quinquefolium) na Asian Ginseng au China ginseng(Panax ginseng) American Ginseng ni  zenya asili ya ubaridi( Ying energy) na Asian Ginseng ni zenye asili ya ujoto(Yang ginseng) , hivyo  basi watu wenye asili ya ubaridi  au waishio maeneo ya baridi  wanashauriwa kutumia Asian ginseng ili waweze kupata joto na wale wenye asili ya joto au waishio maeneo ya joto wanashauriwa kutumia American ginseng kwaajili ya kuongeza baridi katika mili yao. Vinginevyo matatizo makubwa yanaweza kujitokeza hasa kwa watu wenye shinikizo la damu . Mbali na utofauti wote huo lakini mimea yote ina kiungo ...

NI ZAMU YAKO MKAZI WA MWANZA 09/07/2016.

Image
Swali la kujiuliza ni je, unandoto na unatamani itimie, ila hujui jinsi ya kuitimiza? Basi ungana nami tarehe 09/07/2016 ndani ya GOLD CREST HOTEL - Mandela hall,  kuanzia saa sita mchana mpaka saa kumi na moja jioni. Nitakuwepo kukufundisha mbinu mbalimbali za kibiashara na kukutengenezea misingi ya kutimiza ndoto yako.  1. Nitakufundisha mbinu za kuweza kutoka kuitegemea ajira tu na kuanza kujiajiri.  Pia 2. Nitakuonyesha mbinu mbalimbali za kuanzisha biashara. Pia nitakuwa na wenzangu ambao watakusaidia  kukupatia maarifa mbali mbali yatakayo fungua akili yako na kuwa mpya na kisha kuanza kutimiza ndoto yako. Kwaajili ya kukuwekea nafasi, basi tuma jina lako mapema kwenda namba +255 785 494 456. Maana watu watakuwa wengi Ivyo Tuma jina mapema ili tukuwekee nafasi. Unaruhusiwa kumualika ndugu, jamaa na rafiki yako ili nao waje wapate elimu hii BURE. KARIBU SANA.

HABARI NJEMA KWAKO MWANA DAR ES SALAAM

Image
HABARI NJEMA KWAKO MWANA DAR ES SALAAM. Najua kila mtu anatamani kuniona na kujifunza mengi kutoka kwangu.  Sasa fursa ni hii.  NJOO UBUNGO PLAZA, GHOROFA YA PILI, OFFICE NAMBA 202. Nitakuwepo kukufunza juu ya uanzishaji biashara kwa mitaji midogo.  Najua kila mtu anatamani kuwa na biashara yake ila tatizo kubwa limekuwa ni mitaji. Sasa basi, njoo siku ya Ijumaa, Tarehe 24/06/2016 Kuanzia saa 12:00 Mchana mpaka saa 05:00 Jioni. Ili nikupe mbinu hizi adimu kabisa. Njoo, kiingilio ni bure na nitakufundisha bure. Unaruhusiwa pia kuja na mwenzako. By,  Frank A. Ndyanabo - FAN

TANGAZO LA AJIRA

Image
TANGAZO LA AJIRA. NYUMBANI BUSINESS PLAN ENTERPRISES Inakutangazia nafasi ya kazi katika idara ya afisa mauzo kwa watu wote waishio MWANZA. SIFA ZA MUOMBAJI. ••Awe ni muhitimu wa kidato cha nne Au sita. ••Awe na shahada,stashahada au cheti cha Masoko(marketing), Sayansi ya jamii(sociology), usimamizi wa biashara(business administration), fedha (finance), kibenki(banking) KAZI ZA AFISA MAUZO. 1.Kutafuta na kutengeneza masoko mapya ya bidhaa. 2.Kuandaa taarifa ya mauzo kila siku, kwa wiki na mwezi. 3.Kufuatilia na kukusanya mauzo ya kila siku. 4.Kutoa taarifa ya utendaji kazi kwa msimamizi(supervisor) wake kila siku. MSHAHARA MNONO UTATOLEWA TUMA MAOMBI: Tuma maombi yako kwenda kwa Afisa Utumishi wa Nyumbani Business Plan. Email: nyumbanibusinessplan@gmail.com Kwa Mawasiliano zaidi. • +255 753 183 583 • +255 684 459 947 MWISHO WA KUPOKEA MAOMBI NI TAREHE 30/06/2016

ZIFAHAMU NJIA SAHIHI ZA KUBADILI MAISHA YAKO.

Image
ZIFAHAMU NJIA SAHIHI ZA KUBADILI MAISHA YAKO. SEHEMU YA 2. Karibu katika mwendelezo wa mada yetu iliyotangulia ikiwa na sehemu ya kwanza na leo tuko katika sehemu ya pili. Kila mtu anatamani maisha yake yabadilike kutoka alipo na kusonga mbele zaidi. Ila maisha hubadilika pale tu unapotaka yabadilike. Na ili yaweze kubadilika lazima ukubali kupigika kwa ajili ya kuyafanya yabadilike.  Huwezi kulala na kuamka ukakuta yamebadilika. Kwa leo hebu tujifunze njia zingine : 6. Achana na mahusiano yenye kukuumiza. Watu wengi naweza sema ni ving'ang'anizi kwa mambo yasiyo na tija.  Haimaanishi kuwa, kwakuwa umekuwa na mtu au umekuwa ukifanya jambo fulani kipindi cha nyuma basi ni lazima uwe nae au uendelee na mambo hayo maishani mwako. Kukosa jambo fulani ulilolizoea haimaanishi kuwa lazima ulipate.  Au kumkosa mwenzako aliye kuumiza hapo awali haimaanishi kuwa lazima uwe nae maishani mwako.  Kukikosa kitu cha awali ni nafasi nzuri kwako kupata muda wa kusonga mbele k...

UNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA BINTI GETRUDE CLEMENTI?

Image
UNAJIFUNZA NINI KUTOKA KWA BINTI GETRUDE CLEMENTI? Getrude Clement ni binti kutoka Jijini Mwanza, nchini Tanzania.  Na anasoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari Mnarani, ilioko nje kidogo ya mji takribani km 10 au zaidi kutoka mjini. Shule iyo ni ya serikali ni moja kati ya shule za kata zilizoanzishwa kipindi hicho. Getrude ana umri wa miaka 16. Alipata fursa ya kipekee kuongea kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa, akikaribishwa na Mhe. Ban Ki Moon, katibu mkuu wa umoja wa Mataifa kama muwakilishi wa watoto na vijana wote duniani kwa ajili ya kuzungumzia maswala ya mazingira na uchafuzi wake. Baba yake ni Kinyozi na mama yake ni mfanya biashara mdogo mdogo wa nyanya na vitunguu. Getruda Clement, aliweza kuushangaza ulimwengu jinsi alivyo simama mbele ya viongozi mbali mbali nakuweza kuhutubia bila wasi wasi na kwa kujiamini kupita kiasi.  Ujasiri alio nao binti huyu ndio umenifanya niandike maneno haya ili uweze kujifunza kitu fulani. Wewe kama mfuatiliaji mzuri wa...