Posts

Showing posts from March, 2016

JIFUNZE JAMBO HILI KILA SIKU.

Image
Mzee mmoja alianza hofia kuwa yawezekana mkewe kaanza matatizo ya kutosikia vizuri.Hivyo ikambidi amtafute daktari wa familia na kumsimulia mkasa mzima. Baada ya daktari kumsikiliza yule mme vizuri, akamwambia kuwa sasa atahitaji akirudi nyumbani amfanyie jaribio moja mkewe ili majibu yake yaweze kumpa dokta mwanga wa kumsaidia kulitambua tatatizo na yule mama apone. Daktari akamwambia, “ ukirudi nyumbani simama futi 40 kutoka kwa mkeo na kwa sauti ya mazungumzo ya kawaida ongea neno ili uone kama atasikia na kama hatasikia simama karibu futi 30 ukimsogela , kama hatishoshi ongeza zaidi futi 20 mpaka atakapo kusikia” Jioni yake mzee akiwa sebuleni na mama akiwa jikoni anaandaa chakula cha jioni, baba akiwa sebuleni akamwita mkewe na kuuliza, “Mpenzi tuna kula nini leo jioni?” lakini mke hakujibu. Mzee akazidi kusogea futi 30 karibu akamuuliza tena, “Mpenzi tuna kula nini leo jioni?” lakini pia mke hakujibu, mzee akasogea tena fu...

ZINGATIA HAYA KILA SIKU.

Image
ZINGATIA HAYA KILA SIKU. Yaweza kuwa unayafahamu ila hujui umuhimu wake, au unajua ila unayachukulia kawaida sana.  Lazima ufikie mahali ujiulize ni kwa kiasi gani unazitumia mbinu hizi kimaendeleo. Hizi ndio waswahili usema "nondo nzito"  ila mimi nasema ni "funguo tatu muhimu katika maisha yako"  funguo hizi ukipoteza moja wapo basi usitegemee muujiza, Maana mafanikio hayamfuati mtu kama muujiza bali mtu mwenye ndio uyafanya yamtokee kama muujiza kwake.  Na funguo hizi ndio za kutumia ili ufikie pale ulipopalenga. MTANGULIZE MUNGU KILA SIKU: Najua kila mtu ananjia yake ya kuabudu, uwe Mwislam au mkristu unamuabudu Mungu alie juu, basi tambua kuwa ata uwe mjanja namna gani Mungu ndio kilakitu.  Huwezi kufanikiwa bila kumuweka mbele.  Nakumbuka wakati nikiwa shuleni, na nikiwa kiongozi wa dini kwa wanafunzi kimkoa tulikuwa na usemi wetu kuwa "God.... first, education..... Second"  hii inamaana kuwa katika mambo yote utakayoyafanya lazima Mungu umtan...

HACHA KUIHUKUMU NAFSI YAKO

Image
HACHA KUIHUKUMU NAFSI YAKO. Kila mtu analo jambo la kufanya na tunayo malengo ya kutimiza, ila tatizo ni kuwa mioyo yetu imejaa hukumu zisizo za msingi ndio maana tunashindwa kutimiza malengo yetu.  Tunatanguliza kushindwa, aliekwambia kuwa huwezi kumiliki biashara yako nani, nani alikwambia kuwa huwezi kumiliki kampuni?  Nani alikwambia huwezi kuwa kiongozi bora, unafikiri mafanikio watu wanazaliwa nayo?  Yote yanatafutwa hapa hapa duniani.  Hacha kujihukumu bure kuwa huwezi jambo fulani,kwani wewe ni nani usiweze, wanaoweza wana nini cha ajabu? Biashara zetu zinashindwa kustawi kutokana na minyororo iliopo ndani yetu maana tumeifunga kisawa sawa.  Mtu wazo la kufanya biashara au jambo fulani unalo ila hutaki kufanya unategemea nani akufanyie sasa, au unataka jirani yako aje afanye badala yako?  Hachana  na mawazo hayo ya kuifunga nafsi yako, punguza hiyo hukumu na upe mwili wako nafasi ya kufanikiwa, ni kuamini kwamba unaweza, kuondoa mambo yasiyo ...

ZINGATIA HAYA KABLA YA KUANZA BIASHARA YA MTANDAO.

Image
Habari yako ndugu msomaji wa makala zangu za kila siku, ni siku nyingine tena tunakutana hapa nami Mkufunzi wako Frank A. Ndyanabo-FAN Nimekuwa nikikutana na watu mbali mbali, kwa sms, simu, na inbox ya hapa facebook na kwenye mitandao mingine kama kwenye blog yangu ya www.fancompany.blogspot.com, instagram, whatsapp, telegram na LinkedIn wakiniuliza juu ya biashara hii ya mtandao, ila nilikuwa nikiwaambia mambo mbali mbali juu ya biashara hii na mambo ya kufanya ili biashara zao ziweze kunawili na kuwaletea matunda walio yatarajia.  Leo napenda nikushilikishe kitu muhimu sana wewe ndugu yangu mfuatiliaji wa makala zangu hizi, ninaamini kati yenu wapo wanaofanya biashara hii na wengine wako mbioni kuingia na wengine wanatamani kuingia ila hawajuhi waanzie wapi. Kwanza hebu kwa ufupi tufahama biashara ya mtandao ni nini: Biashara ya mtandao au kwa lugha nyingine wanaita biashara ya karne ya 21, ni mfumo wa biashara ambao unamuwezesha mtu kufanya biashara huria kwa kununua bidhaa...

JIFUNZE KUTUMIA PESA

Image
JIFUNZE KUTUMIA PESA. Habari yako ndugu msomaji wa makala zangu za kila siku.  Natumai ni mzima wa afya tele.  Leo nakuletea mada ambayo nimeona ni tatizo kwa watu wengi, hivyo karibu uweze kujipatia somo hili makini na lenye Mwanga wa maisha yetu. Ulisha jiuliza kwa nini maskini wanazidi kuwa maskini zaidi na matajiri wanazidi kuwa matajiri?  Kuna msemo mmoja nimekuwa nikiusikia toka nikiwa mtoto mdogo, kuwa  ukizaliwa maskini basi utakufa maskini na tajiri atazidi kuwa tajiri.  Bado wakaenda mbele zaidi kuwa mwenye nacho atazidi kuongezeawa, hapa tunasema maji ufuata mkondo, haipo siku maji yakapanda mlima.  Kauli hizi zinaweza kuwa kweli au si kweli, Je wewe kutokana na mtazamo wako unaonaje? Kwangu mimi Frank, nasema sio kweli kabisa matajiri wanaendelea kuwa matajiri kwa maana wanajua mbinu sahihi za kutumia pesa hili kutengeneza pesa ndio maana pesa kwao hazikatiki.  Lakini kumbuka watu hao hawakuzaliwa wakiwa matajiri bali nao walikuwa maskin...

JINSI YA KUANZA BIASHARA BILA MTAJI. SEHEMU YA 2

Image
JINSI YA KUANZA BIASHARA BILA MTAJI. SEHEMU YA 2 : Habari yako ndugu msomaji wa makala zangu, natumaini ni mazima wa afya.  Nikukaribishe katika mwendelezo wa darasa hili ambalo leo tunaingia sehemu ya pili, ili kuweza kutazama mambo gani yanaweza kutusaidia ili kuweza kuanza biashara zetu bila mtaji.   Utakuwa nami Mkufunzi na Mshauri wako wa maswala ya biashara, Frank A Ndyanabo. Karibu twende pamoja: TUMIA ELIMU YAKO (USE YOUR KNOWLEDGE) Hili limekuwa ni tatizo kubwa kwa tulio wengi.  Tunapomaliza shule tunawaza kuajiriwa, ulisha jiuliza kiwango cha wahitimu na idadi ya ajira zilizopo? Takwimu zinaonyesha kuwa ajira ni chache ukilinganisha na idadi ya wahitimu wa vyuo nchini hasa apa Tanzania.  Nakumbuka mwaka juzi zilitangazwa nafasi za kazi uhamiaji, walioshiliki katika interview ya hawali walikuwa ni maelufu ya watu mpaka mamlaka husika wakakosa mahali pakuwaweka wakawapeleka uwanjani wa taifa. Sasa jiulize kama interview inafanywa na watu zaidi ya 25...