JINSI YA KUANZA BIASHARA BILA MTAJI. SEHEMU YA 3
JINSI YA KUANZA BIASHARA BILA MTAJI. SEHEMU YA 3. Habari yako ndugu msomaji wa makala hii. Tuko katika mwendelezo wa mada yetu ya, kuanza biashara bila mtaji. Na leo tunaendelea na sehemu ya tatu ya mada hii, leo tutaangalia mambo mawili ambayo unaweza kuyatumia na yakakusaidia katika kuanza biashara. Karibu tujumuike sote. TUMIA UWEZO BINAFSI. Katika hali ya kawaida kila mwanadamu kajaliwa uwezo fulani wa ziada ambao mbali na elimu au kipaji cha kuzaliwa nacho ila anaweza kuwa kajaliwa uwezo fulani binafsi ambao unaweza kuupata kwa kufanyia mazoezi kila mala na ukaweza kubobea katika jambo hilo. Sasa basi kama wewe ni mbobevu katika jambo fulani basi waweza kutumia nafasi hiyo nakuweza kujitengenezea mfereji wa pesa. Mfano: yawezekana wewe ni mbunifu wa mitindo mbalimbali ya mavazi, basi fungua office au kampuni kisha anza kuonyesha umahili wako katika kubuni mavazi na mitindo mbalimbali. Au yawezekana wewe ni mchoraji mzuri, kiasi kwamba ukiamua kuchora b...